ALBINO. kinyume na MTU MWENYE ALBINISM (PWA) MSIMAMO RASMI WA UNDER THE SAME SUN (UTSS)

Similar documents
Towards. New HIV Infections Among Children in Tanzania

CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO TANESCO

ATD Fourth World Registration nº under NGO Act, 2002 P.O. Box 61786, Dar es Salaam Tanzania Phone number:

OKOA FIGO LAKO. Dr Gabriel L. Upunda Dar es Salaam, Tanzania. Free access to read, download and print. Interna

KISUKARI ENGLISH/SWAHILI

OCV SEB Study: Explanatory Model Interview Catalogue (EMIC) Survey Phase: 2, Study Level: IV

"Sikuwahi ambiwa jinsi nilivyokuwa mgonjwa wala Sikuelewa kwamba, Hepatitis C imenidhuru na uharibifu sana. Nildhani kuwa tatizo langu lilikuwa

ANDIKO LA MAELEZO YA KIAFYAJAMII KUSIMAMISHA OVADOSI USAMBAZAJI WA NALOXONE BAINA YA WENZI

GRIZLY. 1 Liter INSECTICIDE. A systemic and contact insecticide for the control of aphids, whiteflies and thrips on roses and tomatoes.

THE Geita Gold Mine. By 2007, about 2 million. GGM extends financial support for institutions fighting HIV/AIDS. Our Vision:

GAIRO HABARI MOTO MOTO

Kenya W1 Smokeless Survey Code: KE1-L Languages: Kiswahili Mode: Face to Face

Kuendesha Gari ukiwa na Ugonjwa wa Kisukari

Acrobat 69% WG READ THE LABEL BEFORE USING (SOMA KIBANDIKO CHA MAELEZO KABLA YA KUTUMIA) KEEP LOCKED OUT OF REACH OF CHILDREN (WEKA MBALI NA WATOTO)

Meltatox 385 EC. Emulsifiable Concentrate FUNGICIDE (KIUAKUVU) KEEP LOCKED OUT OF REACH OF CHILDREN WEKA MBALI NA WATOTO

HIV and AIDS Education Urged for Fishing Areas. Our Vision:

AZIMUT 320 SC. 1 Liter FUNGICIDE. An agricultural systemic and translaminar fungicide for the control of yellow rust and stem rust in wheat

What is Albinism? ALBINISM

NANDI COUNTY ASSEMBLY OFFICIAL REPORT

English - Swahili Dictionary of Meteorological Terms. Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili ya Istilahi za Hali ya Hewa. Kenya Meteorological Department

Understanding and improving malaria diagnosis in health facilities in Dar es Salaam, Tanzania

Regent 50 SC SUSPENSION CONCENTRATE INSECTICIDE (KIUADUDU)

Concept Testing Discussion Guide. Tuko Wangapi Tulizana Phase 2 Bagamoyo, November 7, 12. Location..Gender No of participants

Hospice and Palliative Care. Team Building: Involving the Church

WADAU: Kodi inaongeza bei kondomu

Embe Halijamenywa: The unpeeled mango

INAUGURALDISSERTATION

ENGLISH/SWAHILI BASICS NO SMOKING/USIVUTE SIGARA UNSURE/SINA UHAKIKA

PREVALENCE OF KERATOCONJUNCTIVITIS SICCA IN PATIENTS WITH HIV/AIDS ATTENDING THE COUPLES COUNSELLING CENTRE IN KENYATTA NATIONAL HOSPITAL

Promotion of Community based cultivation of Hibiscus sabdariffa, Moringa oleifera, Adansonia digitata and Aloe vera

CLIENTS SATISFACTION WITH SERVICES FOR PREVENTION OF MOTHER-TO-CHILD TRANSMISSION OF HIV IN DODOMA RURAL DISTRICT

von Nahya Salim Masoud Aus Zanzibar, United Republic of Tanzania Basel, 2015

NACOPHA yaanika fursa

AN EVALUATION OF INTEGRATED INTERVENTIONS TO IMPROVE ACCESS TO MALARIA TREATMENT IN TANZANIA (ACCESS PROGRAMME)

ACCESS TO ART, ADHERENCE AND DRUG RESISTANCE AMONG HIV-POSITIVE PATIENTS IN RURAL TANZANIA


March 23, 2016 PARLIAMENTARY DEBATES 1 NATIONAL ASSEMBLY OFFICIAL REPORT. Wednesday, 23 rd March, The House met at 9.30 a.m.

Tanzanian team. Editor s Note Tanzania is now witness to unprecedented. Big up to Tanzania s anti-stigma law! Issue No. 011 April. 8- April.

OUTCOMES OF URETHRAL STRICTURE AT MUHIMBILI NATIONAL HOSPITAL AND TUMAINI HOSPITAL, DAR ES SALAAM.

TB/HIV KAP SURVEY REPORT

ADEQUACY OF AXILLARY LYMPH NODE DISSECTION IN THE MANAGEMENT OF BREAST CANCER AT KENYATTA NATIONAL HOSPITAL

Ee: JQJIATHAfl THSa* V C. S.,7. KIAIB CKE SO. 122SA8.

von Amani Shao Aus Kilimanjaro, Tanzania Basel, 2015 Originaldokument gespeichert auf dem Dokumentenserver der Universität Basel edoc.unibas.

COME FIRST, GET RIGHT ANSWER

Camilla Wirseen Patna 1 dec Saving Lives

Assisting Birth Attendants in Providing Acceptable Care under Unacceptable Clinical Realities

AIDS PANDEMIC: THE VOICE OF THE YOUTH IN THE KISWAHILI NOVEL

TAARIFA YA UFUATILIAJI NA TATHMINI YA UKIMWI MKOA WA MBEYA

INFORMATION ABOUT ALBINISM. What Is Albinism?

Language Use in the Portrayal of both Women and Men in HIV/AIDS Public Sensitization Texts in the Tanzanian Mass Media

BTS NEWSLETTER.

Management of Sexually Transmitted and Reproductive Tract Infections

MINISTRY OF COMMUNITY DEVELOPMENT GENDER AND CHILDREN WOMEN S INFORMATION CENTRE

GAINING ACCESS TO PROMPT AND APPROPRIATE MALARIA TREATMENT IN THE KILOMBERO VALLEY, TANZANIA: A HEALTH SOCIAL SCIENCE PERSPECTIVE

Wazazi Nipendeni (Love me, parents!) Impact of an Integra5on Na5onal Safe Motherhood Campaign in Tanzania

Habari Gani. Save thedate! June 8th. September 2017

Estimating the Sequestered Load in Plasmodium falciparum Malaria

Understanding Albinism

GRANT DISBURSEMENT REPORT: Donor: Association for Improvement of Mental Health Programs. Beneficiary: KANGEMI COMMUNITY HEALTH VOLUNTEERS GROUP

BTS NEWSLETTER. Chair s Report How we started, What we do now The way ahead - see page 14. "Request for help as BTS enters a new phase"

A REVIEW OF MANAGEMENT OF FEMORAL NECK FRACTURES IN KENYATTA NATIONAL HOSPITAL BY DR. DAN F.OJ OCHIEL M.B.CH.B (NAIROBI)

Normal Biosynthesis of Melanin

Children with Albinism in Africa: Murder, Mutilation and Violence 56 APPENDICES. APPENDIX A: Why We Prefer Person With Albinism to Albino

PUBLIC AND ENVIRONMENT HEALTH ACT, NO. 11 OF 2012 ARRANGEMENT OF SECTION PART ONE PRELIMINARY PROVISIONS

The Impact of Value-Orientations on Cross-cultural Encounters and Mediation: A Survey in Tanzania s Educational System

Key words: mobile literature, communication, billboards, murals, AIDS, Kiswahili sayings

SOCIO-ECONOMIC STATUS, KNOWLEDGE, AWARENESS AND ATTITUDES OF THE SWAHILI COMMUNITY IN RELATION TO DIETARY HABITS, OBESITY AND LIFESTYLE DISEASES

2. The clinician will know how to manage common pediatric ocular diseases

Contents. Opening Remarks: 1. Part1 (GGG, TB, GDF, Polio, IAVI and Vaccination): 8. Part2 (Nutrition and Refugees): 19

THE IDEA STUDY DEMENTIA TRAINING FOR HEALTHCARE WORKERS 2014

Patient Symptoms- What They Might Mean. Sarah Dougherty Wood, OD, MS, FAAO Heart of America, February 2011 Paraoptometric Lecture

Working together to eliminate cyanide poisoning, konzo and tropical ataxic neuropathy (TAN).

Clinical Pearls: Infant vision examination Deborah Orel-Bixler, PhD, OD University of California, Berkeley School of Optometry

Albinism: From genotype to phenotype

PREVALENCE OF CHRONIC RHINOSINUSITIS IN CHILDREN WITH DYSPEPSIA AT KENYATTA NATIONAL HOSPITAL AND GERTRUDE S CHILDREN S HOSPITAL PRINCIPLE RESEARCHER:

People with albinism in Niger are part of the category of people with disabilities, but data about them remain unknown to date.

INVESTIGATION. Quality of life in patients with oculocutaneous albinism*

INFANTILE EXOTROPIA. Lionel Kowal

Key Populations Newsletter

Transillumination of iris and subnormal visual

PLEASE SCROLL DOWN FOR ARTICLE

BASIC SCIENCE LECTURES

Thursday, 21 October :31 - Last Updated Wednesday, 24 November :23. Albinism -and Other Genetic Disorders. of Pigmentation 1 / 10

Title: Characterisation of Abnormal Optic Nerve Head Morphology in Albinism Using Optical Coherence Tomography

Children's Eye Assessment

ADEQUACY OF AXILLARY LYMPH NODE DISSECTION IN THE MANAGEMENT OF BREAST CANCER AT KENYATTA NATIONAL HOSPITAL

A lbinism is a heterogeneous, genetically determined disorder

Concentric Macular Rings Sign in Patients With Foveal Hypoplasia

Situation Assessment HIV Counseling and Testing in Iringa Region. March 2009

Minimally invasive treatment of traumatic high rectovaginal fistulas

X linked ocular albinism in Japanese patients

Identifying Human Albinism: A Comparison of VEP and fmri

Prepared by Tanzania Media Women s Association (TAMWA)

INHERITED RETINAL DISEASE. The Rod/Cone Dichotomy. Case History/Entrance Skills. Health Assessment 9/4/18. Hereditary Retinal Diseases Epidemiology

Sources of Donor Organs & Their Ethical Implications. Baraka M. Morris, BScN, RN, MBE

EMPEROR'S COLLEGE MTOM COURSE SYLLABUS HERB FORMULAE I

A Japanese Family With Autosomal Dominant Oculocutaneous Albinism Type 4

Dr Casey Ung. Ophthalmologist Dunedin Hospital Eye Clinic Marinoto Clinic & Specialists Dunedin

KIVULINI WOMEN S RIGHTS ORGANIZATION ANNUAL PROGRAM REPORT 2013

Discrimination Against Women and Girls With Albinism in Malawi

Transcription:

ALBINO kinyume na MTU MWENYE ALBINISM (PWA) MSIMAMO RASMI WA UNDER THE SAME SUN (UTSS) Kama kikundi cha kutetea heshima ya watu wenye albinism, UTSS inapendelea kusema Mtu Mwenye Albinism 7 (PWA) na maneno mengine mbali mbali yanayofanana na hayo kuliko kusema albino. Hii siyo tu kwa kuwa kihistoria matumizi ya neno albino, yanaonesha udhalilishaji lakini pia kwa sababu matumizi ya maneno Mtu Mwenye Albinism, yanatanguliza utu wa mtu kwanza kabla ya hali yake ya maumbile. Baada ya kusema hayo, tunaelewa kwamba dunia sasa hivi ipo kwenye kipindi cha mpito kutoka kwenye matumizi ya neno albino hadi matumizi ya watu wenye albinism hivyo mara chache chache, tunaweza kulazimika kutumia neno albino kama matumizi ya watu wenye albinism hayatakwenda sanjari na ujumbe muhimu unaotolewa. SABABU ZA KUWA NA MSIMAMO WETU Shirika la Under The Same Sun (UTSS) linaona ni vyema na ni sahihi kutumia neno albinism kwa watu wenye ulemavu huo. Tunapaswa kumwita mtu kwa kutumia jina lake na siyo kutumia hali yake aliyozaliwa nayo. Maneno kama vile zeruzeru, albino, mzungu na mengine mengi ni maneno yanayoonyesha dharau, ubaguzi, unyanyapaa, udhalilishaji na yanaondoa utu kwa watu wenye albinism. Albinism ni nini? Shirika la Under The Same Sun (UTSS) linaona ni vyema na ni sahihi kutumia neno albinism kwa watu wenye ulemavu huo. Tunapaswa kumwita mtu kwa kutumia jina lake na siyo kutumia hali yake aliyozaliwa nayo.

Maneno Kama vile zeruzeru, albino, mzungu na mengine mengi ni maneno yanayoonesha dharau, ubaguzi, unyanyapaa, udhalilishaji na yanaondoa utu kwa watu wenye albinism. Hali hii ya kurithi - Albinism ipo duniani kote. Albinism inaathiri watu wa mbari au jamii zote bila kujali rangi au asili yao kila mbari/jamii ina watu wenye Albinism. Mtu anakuwaje na albinism? Kila mtu mwenye albinism huwa amerithi kutoka kwa wazazi wake wote baba na mama. Wazazi wote wenye albinism, wawe na ulemavu huo au la watakuwa na jeni za sifa bainishi za albinism kabla ya kuzaliwa kwa mtoto mwenye albinism; Wazazi wote wanapokuwa na tabia bainishi za albinism (na hakuna mzazi aliye na ulemavu huo) kuna uwezekano wa moja kati ya nne (au 25%) ya kila ujauzito kuwa mtoto atazaliwa na albinism; Watoto wenye rangi ya asili ya kawaida waliozaliwa na wazazi hao nao watakuwa na jeni za sifa bainishi za albinism. Watoto hao nao watawarithisha sifa bainishi hizo watoto wao. Kwa nini watu wenye albinism wanakuwa na rangi angavu sana? Watoto wengi wenye albinism wanazaliwa na wazazi wenye nywele na rangi ya macho ya asili ya mbari (race) yao. Watu wenye albinism wanashindwa kutengeneza kiasi cha kawaida cha rangi ya asili kiitwacho melanin Ndiyo maana watu wenye albinism wana rangi asili ndogo au hawana kabisa kwenye macho yao, ngozi, nywele au kwenye yote yaliyotajwa hapo juu. Aina za albinism Albinism inayoathiri macho tu. Ulemavu huu unaoitwa ulemavu wa macho (OA), si wa kawaida sana. Huwapata sana wanaume. Watoto wenye albinism wanaweza kuwa na rangi ya ngozi au nywele ya kawaida lakini iliyopauka kidogo kuliko ile ya ndugu wengine katika familia. Albinism inayoathiri ngozi, nywele na macho hujulikana kama OCA. Hii ni albinism inayopatikana sana nchini Tanzania. Kwa kutumia kipimo cha vinasaba (DNA), aina nne za albinism ya OCA zinabainishwa. Hizi ni OCA1, OCA2, OCA3 na OCA4; Baadhi ya aina hizi zimegawanywa katika aina nyingine ndogo ndogo kutokana na tofauti ya kiwango cha rangi/melanin alichonacho mtu.

Albinism yenye ziada: Watafiti pia wamegundua aina ya albinism yenye sifa bainishi za ziada. Hali hii ya albinism inayoitwa HPS unahusishwa na matatizo ya kutokwa na damu na kuvilia kwa damu. Kwa baadhi ya watu wenye albinism yenye sifa bainishi za ziada wanakuwa na maradhi ya mapafu na matumbo. HPS si aina ya kawaida sana ya albinism, lakini mtu mwenye albinism atashukiwa kwamba ana HPS kama ataonyesha albinism yenye kuvilia au hali ya kutokuwa na damu isiyokuwa kwa kawaida. CHANGAMOTO ZA ALBINISM 1. Matatizo ya uoni, Tiba na Urekebishaji Watu wenye albinism mara nyingi wana matatizo ya kuona yasiyoweza kurekebishwa kabisa kwa miwani. Matatizo ya uoni kwa watu wenye albinism yanatokana na ukuaji usio wa kawaida wa mishipa ya fahamu inayounganisha macho na ubongo unaosababishwa na ukosefu au uhaba wa rangi asili/melanin. Kiwango cha matatizo ya kuona kinatofautiana kutokana na aina mbalimbali za albinism ya watu wenye ulemavu huo. Kwa ujumla hawaoni vizuri. Hata hivyo wengi wao wanaweza kutumia uwezo wao mdogo wa kuona kufanya kazi nyingi ikiwemo kusoma. Watu wengi wenye albinism hawatumii maandishi ya nukta nundu Braille Watu wachache wenye albinism wana uwezo wa kuona na kuendesha gari. 2. Matibabu na Urekebishaji Watu wenye albinism mara nyingi wana mchanganyiko wa mojawapo kati ya haya: JINA LA HALI MATIBABU UREKEBISHAJI (unapopatikana) Nystagmus Mwendo wa macho wa mara kwa mara, upande mmoja hadi mwingine au kwa kuzungukazunguka Siku hizi upasuaji unapunguza lakini hautibu kabisa tatizo hilo, kitaalamu linajulikana kama Nystagmus Strabismus: Makengeza Kukosa uwiano wa misuli ya macho Kwa matatizo ya macho ya trabismus kunaweza kurekebishwa

(esotropia ), macho ya kupooza au jicho linalotokeza nje (exotropia) Photophobia: Mwanga mkali wa upigaji picha au Mweko: Matatizo ya kuangalia kwenye mwanga mkali hasa kwa macho yaliyopooza esotropia au makengeza, upasuaji unaweza kusaidia kuona kwa kupanua uga wa uonaji (eneo ambalo macho yanaweza kuona wakati wa kuangalia mahali pamoja) Watu wenye albinismwanahitaji kuona kama mtu mwingine yeyote. Miwani ya jua au lenzi nyeusi husaidia mwanga wa nje. Kwa ndani ya nyumba, ni muhimu kuweka taa za kusomea usawa wa bega kuliko mbele. Kuona Mbali au Karibu (astigmatism) iliyochanganyika na mwonekano uliovurugika. Foveal hypoplasia Kwa kawaida dosari katika jicho/lenzi inayozuia fokasi sahihi kama kuona kiwi wakati wa kuona mbali au karibu Ukuaji usio wa kawaida wa sehemu ya ndani ya jicho inayopokea mwanga inayojulikana kama mboni ya jicho (retina). Kuna vifaa mbali mbali vya kusaidia uoni wa watu wenye albinismikiwa ni pamoja na miwani yenye lenzi iliyogawanyika sehemu mbili * moja ya kusomea yenye darubini ndogo iliyofungwa juu yake na sehemu nyingine ya kawaida (Bifocals) Watu wenye albinismwanahitaji kuona kama mtu mwingine yeyote. Miwani ya jua au lenzi nyeusi husaidia mwanga wa nje. Kwa ndani ya nyumba, ni muhimu kuweka taa za kusomea usawa wa bega kuliko mbele. Optic nerve misrouting Mishipa ya fahamu ya mwanga inabadilisha mwelekeo wa ishara za fahamu kutoka kwenye

retina kwenda kwenye ubongo bila kufuata mikondo ya kawaida ya mishipa ya fahamu. *Baadhi ya nchi zinaruhusu watu wenye albinism kutumia miwani ya lenzi mbili 3. Matatizo ya ngozi na namna ya kuyazuia Watu wenye aina nyingi za albinism wanahitaji kuchukua tahadhari kuepuka kuathirika kwa ngozi zao na mionzi ya jua. Athari za ngozi zinaweza kuepukwa kwa kujipaka mafuta ya kuzuia mionzi ya jua, kuvaa kofia na nguo ndefu za kukinga mionzi ya jua. 4. Changamoto za matibabu na namna ya kuziepuka Katika nchi nyingi, watu wenye albinism wanaishi umri wa kawaida na wana matatizo ya matibabu ya kawaida kama watu wengine wowote wale. Wale wenye hali ya athari za ziada kama vile HPS watakuwa na maisha mafupi kutokana na maradhi ya mapafu au mabadiliko mengine mahususi. Kwenye nchi zenye jua kali na joto au hali ya hewa ya kitropiki kama Tanzania, watu wenye albinism wasiochukua hatua za kulinda ngozi zao wanaweza kupata saratani ya ngozi zinazotishia maisha yao. Watu wenye albinism katika nchi hizo hawana budi kulinda ngozi zao ipasavyo kama vile kujipaka mafuta ya kujikinga na mionzi ya jua ya kiwango cha kuanzia angalau SPF 20 na nguo ndefu zitakazowasaidia kufurahia kufanya shughuli za nje na maisha ya kawaida. 5. Changamoto za Kijamii na namna ya kuziondoa Watu wenye albinism wapo katika hatari ya kutengwa kwa sababu hali yao mara nyingi haifahamiki. Unyanyapaa wa kijamii unaweza kutokea, hasa ndani ya jamii ambamo ndugu na jamaa wana ngozi na sura zenye rangi asili. Familia na shule hazina budi kufanya juhudi za kuwajumuisha watoto wenye albinism katika shughuli za vikundi au za pamoja. Mawasiliano na watu wengine wenye albinism au wengine wenye watu wenye albinism kwenye familia zao wanaweza kusaidia zaidi.

6. Changamoto za kielimu na namna ya kuzikabili Kutokana na udhaifu wa kuona, watu wengi wenye albinism hawawezi kusoma ubaoni katika hali ya madarasa ya kawaida; Walimu na wakufunzi hawana budi kufanya juhudi ya ziada kupanga upya darasa ili kuwaweka mbele na karibu zaidi ya ubao; Upangaji upya huu lazima ufanyike ili watu wenye albinism wasiuangalie mwanga wa jua wakati wa kusoma ubaoni; Kuimarisha upangaji upya, ubao lazima uwe mweusi daima ili mwonekano wa chaki nyeupe uongeze uwezo wa kusoma; Kama upangaji upya utashindikana, walimu na wakufunzi wawe tayari kutoa nakala za maelezo ya somo na kumgawia kila mwenye albinism darasani mwao; Mitihani, maelezo ya somo la mwalimu na vitini vingine vilivyochapwa/vilivyotolewa nakala havina budi kueleweka na vyenye maandishi makubwa kiasi; Muda wa ziada lazima utolewe kwa watu wenye albinism wakati wa kufanya mitihani; (Inapendekezwa kuongeza nusu ya muda halisi). Hii ni muhimu sana hasa kama maswali ya mtihani yatatolewa kwa maandishi madogo au ya kawaida, na kama nakala za mitihani zilizotumika zimefifia; Kwa msaada wa kila siku walimu na wakufunzi wataona kuwa inafaa zaidi kumpangia mwanafunzi mmoja (asiye na albinism) mwenye uwezo wa kimasomo kwa kila mwanafunzi mwenye albinism wakati wa kujifunza; Maelezo zaidi ya kina kwa ajili ya walimu na wakufunzi wa watu wenye ulemavu huu yanapatikana kwenye kitabu cha MWONGOZO ambacho ni rahisi kusoma. Nakala zinaweza kupatikana kwa kuwasiliana na UTSS. Kwa maelezo zaidi wasiliana na UNDER THE SAME SUN UTSS TANZANIA PO Box 32837 DSM, Tel: +255222780224 Fax +255222780224 Email: info@utsstz.com

Chimbuko la maelezo NOAH The National Organization for Albinism and Hypo-pigmentation http://www.albinism.org VISION FOR TOMORROW The Vision for Tomorrow Foundation www.visionfortomorrow.org MAONI YA KITAALAMU Dr. Murray Brilliant, Geneticist. Interview on Discovery Channel s My Shocking Story: Albino Crisis / Part 2 (12:55 to 13:38). See http://www.yourdiscovery.com/web/ my-shocking-story/first-5-minutes/ SABABU ZINAZOELEZEA MSIMAMO WETU Albino o Albino ni neno linalomwelezea mtu na hali yake. o Kwa hiyo kutumia neno albino ni sawa na kumlinganisha mtu huyo na maumbile ambayo yanaonekana dhahiri: albinism o Kumlinganisha mtu na hali yake ya maumbile ni kinyume cha jitihada za kimataifa za kuheshima utu wa watu wote. Albinism o Haisababishi ukosefu wa rangi asili kwenye macho, ngozi, nywele na macho tu o Bali pia inasababisha kutokamilika kwa ukuaji wa mfumo wa jicho ***Matokeo yake ni kwamba watu wenye albinism wana ulemavu wa macho ambayo yanawafanya watambulike kisheria kuwa watu wasioona Nchini Canada na nchi nyingine duniani watu wenye albinism wamesajiliwa kama watu wasioona na ni sehemu ya jamii ya watu wenye ulemavu

Mambo yanayoweza kukusaidia kuuelewa msimamo wetu Negro: Neno hili likiwa peke yake halina madhara. Katika baadhi ya lugha linamaanisha mweusi. Lakini historia imedhihirisha kuwa neno hilo kwa watu waliokuwa wanaitwa hivyo limeonekana kuwa ni utambulisho unaodhalilisha. He, we (weka hali ya maumbile ya mtu!) : Iwapo siyo sahihi kumwita mtu huku nikipaza sauti kuvuka barabara: He! we kipofu! Au He! We mwenye ugonjwa wa moyo! basi kumwita mtu kwa kupaza sauti akiwa ng ambo ya barabara, He! We albino! vile vile ni udhalilishaji. Endapo dunia inawaheshimu watu wote, hakuna mtu yeyote mwenye ulemavu ambaye anapaswa kupewa jina linaloelezea hali yake ya kurithi. Maelezo mwanana: Huyu ni albino: Kinyume na kile unachokiona kwenye filamu au unachokisikia mitaani, siyo jambo la heshima kumwambia rafiki yako, "He, mwangalie yule karani albino!" Jinsi dunia inavyozidi kuendelea, na heshima inavyotolewa kwa watu wote, hakuna mtu yeyote mwenye ulemavu anayestahili (hata kwa sauti ya upole sana au nia njema kabisa) kuitwa jina linaloelezea hali yake ya ulemavu. Ni bora kusema, kwa mfano, nadhani karani yule ana albinism. Ukiwa na uhuru wa kuongea, lugha inakuwa njia rahisi na yenye nguvu ya kusaidia wengine. ---Timiza wajibu wako leo hii! Toa mchango wako ili kuheshimu utu wa mtu!